Akizungumza katika kipindi cha Hot Mix cha East Africa Television akijibu swali la mtangazaji wa kipindi Adrian Stepp,
msajili wa vyama vya siasa nchini amedai kuwa ikibainika kuwa CHADEMA
ndio waliohusika katika kulipua bomu katika mkutano wao wa 15/06/2013
atakifuta.
Alipoulizwa kama itathibitika kuwa CCM ndio walihusika kulipua bomu hilo
amedai kuwa hawezi kukifuta kwakuwa kwa kufanya hivyo itakuwa ni
kufanya mapinduzi ya kalamu. Kwamba CCM ikifutwa nchi itaparaganyika na
kusababisha jeshi kuchukua nchi.
MY TAKE:
Hii ni dalili ya wazi ya msajili kuwa na double standards katika maamuzi
yake juu ya vyama vya siasa, na hii inathibitisha madai ya muda mrefu
kuwa amekuwa akifanya kazi kwa kuipendelea CCM. Kama angekuwa hafanyi
kazi kwa kupendelea na kulipa fadhila basi angekuwa tayari kukifuta
chama chochote kitakachobainika kulipua bomu katika mkutano wa CHADEMA
Arusha
No comments:
Post a Comment