Thursday, 11 July 2013
Tuesday, 9 July 2013
AGNESS MASOGANGE AKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA
HATIMAYE
wale Wanawake wawili walionaswa na madawa ya kulevya Afrika
kusini wametambuliwa kuwa ni mabinti wa KITANZANIA ..
Mabinti hao wanadaiwa kuingiza shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8 nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.
Akizungumza na mwandishi wetu jana, Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Geofrey Nzoa, alisema haijafahamika wanawake hao wanatoka mikoa gani.
Kamanda Nzoa aliwataja wanawake hao kuwa ni Agnes Jerald (MASOGANGE) ambaye alisema hajapiga hesabu ya umri wao, ila alizaliwa mwaka 1988 kwa maana hiyo ana umri wa miaka 25 na Melisa Edward ambaye alisema amezaliwa mwaka 1989 kwa maana hiyo atakuwa na umri wa miaka 24. Wawili hao bado wanaendelea kuhojiwa na polisi wa Afrika Kusini.
Alisema Jeshi la Polisi Nchini kwa upande wake linaendelea kufanya uchunguzi kubaini kama dawa hizo walitoka nazo wapi na pia linawasaka watu ambao watakuwa ndiyo wamiliki wa dawa hizo.
Jumapili iliyopita mtandao huu ulipata taarifa za kukamatwa kwa dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani hiyo nchini Afrika Kusini wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania.
Taarifa hizo zilionyesha kuwa wanawake wawili walikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Oriver Tambo uliopo eneo la Kempton Park siku ya Ijumaa wiki iliyopita wakitokea Tanzania.
Wanawake hao walikamatwa na maofisa wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini wakiwa na masanduku sita ambayo yalipokaguliwa yalikutwa na takribani kilo 150 za dawa hizo ambazo pia zinajulikana kama ‘Tik’ zikiwa na thamani ya bei ya mtaani ya Randi milioni 42 sawa na Sh. bilioni 6.8.
Baada ya kukamatwa na dawa hizo wanawake hao walikabidhiwa polisi. Tukio hilo linatoka takribani wiki moja baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Juni 28, mwaka huu kutangaza kuwa tatizo la dawa za kulenya hivi sasa ni janga la kitaifa nchini.
Alisema kumekuwa na wimbi kubwa la Watanzania wanaojiingiza katika biashara haramu ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi na kwamba, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, watuhumiwa 10,799 walikamatwa kwa kujihusisha na dawa hizo.
Pia alisema katika kipindi hicho, Watanzania 240 walikamatwa katika nchi za Brazil, Pakistan na Afrika Kusini, na hivyo kuharibu taswira ya nchi na kusababisha Watanzania wasio na hatia kupata usumbufu na masharti magumu wanapotaka kusafiri kwenda nchi mbalimbali duniani.
Pinda alisema mwaka huu pekee kumekuwa na ukamataji mkubwa wa dawa za kulevya katika eneo la kimataifa la Bahari ya Hindi karibu na Tanzania.
Alisema hivi sasa mikate, maandazi na askrimu zinazouzwa kwenye shule za msingi, zinawekwa dawa za kulevya.
Alisema vitendo hivyo vinafanya vijana wengi wa shule za msingi na hata sekondari kuwa na tabia za ajabu, ikiwamo kuingia darasani wakiwa na kiatu kimoja mguuni, mkufu wenye nyembe na kidani chenye nyembe kifuani.
Melezo Kwa hisani ya Nipashe.
Read more: http://talkbongo.blogspot.com/2013/07/agness-masogange-akamatwa-na-madawa-ya.htm

Sunday, 7 July 2013
MBOWE AFANYA MAZUNGUMZO NA MAAFISA WA IKULU YA MAREKANI
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe
ambaye alialikwa kushiriki dhifa ya Kitaifa Ikulu wakati wa ziara ya
Rais Barack Obama wa Marekani alifanya jambo kubwa muhimu kwa
mustakabali wa Demokrasia hapa nchini.
Mwenyekiti huyo ambaye pia ni
Kiongozi Rasmi wa upinzani bungeni alipata fursa adhimu ya kufanya
mazungumzo ya Faragha na maafisa wa Ikulu ya Marekani walioambatana na
Rais Barack Obama.
Mpaka sasa kilichozungumzwa na
Kiongozi huyo anayeongoza chama kinachopendwa na watanzania wengi zaidi
hakijawekwa bayana ingawa wachunguzi wa mambo wanasema yalikuwa
mazungumzo nyeti na muhimu kwa mustakabali wa demokrasia na amani ya
Tanzania.
Kim Kardashian ashawishiwa na mama yake kuuza picha ya mtoto wake kwa dola milioni 4!
LOS ANGELES
Mama wa staa Kim Kardashian, Kris
Jenner,amemshawishi mwanaye kuuza picha ya kitoto chake kichanga kwenye
chombo cha habari kwa dola milioni 4, Hollywood Life limeripoti.
Vyanzo vya karibu na staa huyo vimesema
Kim amekuwa wazi kuuza picha ya kwanza kabisa ya binti yake (North
West), lakini Kanye West amekuwa akipinga kuhusu suala hilo na kutaka
utambulisho wa mwanaye kuwa siri.
Chanzo karibu na familia hiyo kinadai
kwamba Kim anapingana na wazo la Kanye West huku akilinganisha hali yao
na waliyokuwa nayo wakina Angelina Jolie na Brad Pitt, ambao waliuza
picha za kwanza za wanao mapacha kwa dola milioni 15.
Shagor
GAIDI MWENYE URAIA WA NCHI NYINGI AKAMATWA BONGO!!
Jeshi la Polisi nchini limemtia
mbaroni mtu mmoja mjini Mbeya anayedaiwa kuhusika na vitendo vya ugaidi
akiwa na hati mbili za kusafiria, na mwingine Mtanzania adakwa akidaiwa
kusaidiana naye.
Mtu huyo aliyekamatwa wilayani Kyela, pia anatuhumiwa kuhusika na vitendo vya ugaidi nchini Uingereza.
Akizungumza na waandishi wa habari
jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI),
Robert Manumba, alisema mtuhumiwa huyo alikuwa anatumia majina mawili
tofauti kwenye hati za kusafiria na alikuwa akijaribu kuvuka mpaka wa
Tanzania kuelekea Malawi.
Alisema mtuhumiwa huyo alitumia hati
ya Tanzania yenye namba AB 651926 yenye jina la Adil Ally Patel na hati
ya Uingereza yenye namba NO 51555382 yenye jina la Iqbal Hassan Ally.
Manumba alisema hati ya Tanzania aliyokamatwa nayo ni kati ya hati 26 zilizoibiwa kwenye Ofisi za Uhamiaji mwaka mmoja uliopita.
Alisema mshukiwa wa ugaidi alikuwa
akisaidiwa na Mtanzania mmoja ambaye hakumtaja jina na baada ya
kukaguliwa kompyuta mpakato (laptop) yake ilikuwa na maneno ya uchochezi
ya kidini kuhusu imani tofauti.
Manumba alisema aliwasiliana na
Serikali ya Uingereza kuhusu hati ya mtuhumiwa huyo na kuelezwa kuwa ni
halali na kufahamishwa kuwa mtu huyo wanamtafuta kwa tukio la ugaidi
nchini Uingereza.
Alisema kuna Mtanzania mwingine
ambaye hakumtaja jina, alikamatwa kwa kuhisiwa kujihusisha na mtuhumiwa
huyo wa ugaidi ambaye baada ya kukaguliwa pia alikutwa na kompyuta yenye
maneno ya uchochezi dhidi ya dini isiyomhusu.
Alisema mtuhumiwa huyo alijitambulisa kuwa ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo kimoja kilichopo nchini Sudan.
Manumba aliwataka wazazi kuwa
waangalifu na vijana wao wanaokwenda kusoma nje ya nchi kwa kuwa baadhi
yao hurubuniwa na kujiingiza katika mambo yanayohusiana na ugaidi.
Aliongeza kuwa polisi wana uhakika
kwamba kuna baadhi ya vikundi vya kigaidi ndani ya nchi ambavyo vina
mipango ya siri ya kutekeleza ugadi nchini.
Aliwataka Watanzania kuwa waangalifu
wakati polisi ikifanya kazi yake ya uchunguzi na kuonyesha kuwa hali ya
usalama si nzuri nchini kutokana na matukio ya kihalifu yanayoendelea.
Aidha, alisema polisi inaendelea na
uchunguzi dhidi ya matukio ya mlipuko miwili ya mabomu iliyotokea mkoani
Arusha na lile la kuuawa kwa Padri Evarist Mushi, Zanzibar.
Alisema matukio hayo yameonyesha sura mbaya kwa Tanzania ya kuwepo kwa tishio la ugaidi.
Alisema uchunguzi utakapokamilika washitakiwa watafikishwa kwemnye mikono ya sheria kuhukumiwa kwa makosa ya jinai.
Aliongeza kuwa taarifa zitakazokuwa
zikitolewa na raia wema zitasaidia polisi kurahisisha uchunguzi na
kuwakamata wahusika kwa wakati.
Manumba ametahadharisha kuwa ongezeko
la uhalifu nchini limekuwa likihusisha baadhi ya wananchi kutumika
vibaya na wavunjifu wa amani.
Alisema kufuatia matukio hayo, baadhi
ya watuhumiwa wanashikiliwa na baada ya uchunguzi kukamilika hatua kali
zitachukuliwa dhidi yao.
“Hii ni sifa mbaya Watanzania
wanapaswa kujiepusha na vishawishi vya aina yoyote vitakavyopelekea
kuvunjika kwa amani iliyopo tangu kupatikana kwa uhuru wa Tanzania,”
alisema.
Katika matukio ya kigaidi yaliyotokea
siku za hivi karibuni watu watatu walikufa na zaidi ya 70 kujeruhiwa
baada ya kurushwa bomu kanisani na mtu asiyefahamika katika kanisa la
Katoliki Jimbo Kuu la Arusha wakiwa wamejumuika katika uzinduzi wa
Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti.
Katika tukio jingine jijini humo,
bomu lilipuka kwenye mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) eneo la Soweto kata ya Kaloleni mkoani Arusha.
Katika tukio hilo watu watatu
walifariki dunia kutokana na mlipuko wa bomu wakati chama hicho kikiwa
kwenye mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi wa madiwani.
Wakati huo huo Manumba alisema polisi
jijini Dar es Salaam limekamata meno ya tembo 347 katika eneo la Kimara
ambayo yanaamika yamepatikana kwa njia za kijangili katika mbuga za
Tanzania.
Alisema mbali na nyara hizo, kuna
meno mengine ya tembo 788 yalikamatwa nchini Malawi katika mji wa Mzuzu
na kwamba inaamika kuwa yalisafirishwa kutoka Tanzania kama mzigo wa
saruji kutoka katika kiwanda cha Saruji Mbeya.
Manumba alisema polisi nchini
wanafanyakazi kwa kushirikiana na polisi wa kimataifa kuhakikisha kuwa
ukweli wa matukio yanakuwa wazi na uchunguzi ukikamilika wahusika
watafikishwa katika vyombo vya sheria.
HUYU NDIYE ASKARI WA KIKE MZURI AMBAE HAJAWAHI TOKEA KABLA
Nchini kenya inasadikika kuwa huyu ndiye mwanamke polisi ambae ni mzuri kuliko wote waliowahi kutokea nchini kenya
CHEKI PICHA KINACHOENDELEA TAMASHA LA MATUMAINI: MBWIGA WA CLAUDS FM AKATA MAUNO NA MSONDO
Mbwiga
Mbwiguke wa Clouds FM akikata mauno wakati Bendi ya Msondo Ngoma ikitoa
burudani katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2013. Mbwiga alikuwa
kivutio kwa wananchi waliokuwa katika tamasha…
Bendi ya Msondo Ngoma ikiwapa burudani wananchi ndani ya Uwanja wa Taifa katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2013.
Uwanja wa Taifa kwenye Tamasha la matumaini sasa hivi.
"NI KWELI KWAMBA NAVUTA SANA BANGI".....T.I.D
Mtangazaji
wa kipindi cha The Sporah Show, Sporah Njau hivi karibuni alijikuta
katika wakati mgumu alipofanya interview na muimbaji mahiri nchini,
Khalid Mohamed aka TID kwenye show hiyo kutokana na maswali yake
yaliyogusa mambo ya ndani ya mkali huyo.
Sporah alimuuliza maswali yaliyogusa masuala mazito katika maisha ya msanii huyo ikiwa ni pamoja na shutuma kuwa anatumia madawa ya kulevya, tabia yake inayotafsiriwa kama ya dharau, kuwa na hasira, kupungua kwa afya yake na suala la kifo cha aliyekuwa rafiki yake, Albert Mangweha.
TID alikuwa akijieleza zaidi kwa lugha ya Kiingereza huku akitumia Kiswahili kidogo. Haya ni baadhi ya masuala aliyoulizwa na kujibu:
Kuhusu sababu ya kifo cha Ngwair
I don’t have a crew kwa sababu he was away, he was in South Africam actually in Johannesburg. He was on tour it was actually a proper time we wanted him to go that big baada ya ile nyimbo tuliyofanya ‘No Beef’ and it was getting a lot of airplay, so we thought that could be the right time for him.
We gave him a concert abroad ili apate exposure so when he comes back he is gonna be on the right time. Lakini ndio hivyo bahati mbaya we just heard like he was unconscious then he stopped breathing, they took him to hospital and he was lastly pronounced dead.
Sasa mimi hata sijui, I am in Tanzania and I haven’t slept for the past two months kwahiyo sasa sielewi ni nini tatizo limeenda. Wao wamesema it’s a sudden death hivyo ndivyo wameandika kwenye certificate yake ya death. I am gonna miss this guy, damn only God knows how much.
Kuhusu lini ataacha kuwa mtu wa sifa.
This is whom I am, sometimes it’s hard for people to understand, me I am not like them, I am different, I am the other guy they see me on TV so when they think I have Misifa, maybe that’s the attitude that I was born with. It’s very hard to explain, it’s very hard to make everybody like you while you are on the spotlight, it’s impossible. And sometimes I have to get it along, all my tweets are everywhere, it’s crazy. When I’m saying am taking a shower right now, people say ‘why are taking shower right now’ they have to comment about me.
Kuhusu shutuma kuwa anatumia madawa za kulevya.
People say a lot of things about me, they were just trying to exaggerate my life. Yes I’m smoking marijuana, that’s my sensitive thing. Hata kama promoter amenikuta nimelala, I had too much to drink., I am tired of the show, nimesafiri siku nzima, nimetoka zangu Dar es Salaam kwenye msiba, I have to be tired, I am a human being, I don’t have any access to drugs in the UK, how can I get drugs here? That’s impossible but to me it’s because I am on the spotlight and everybody is tryna get the advantage of it.
And I really don’t know who are they, do they like me? Do they fancy my fortune? Do they wanna be like me? Do they appreciate the talent I have been giving for all these years? Au do they want to come around and make a point? So I am gonna do what I do best, give them right tunes, connecting my music to the world like what I am doing right now. These is more like a third time me and you (Sporah) we are talking right here, people with drugs don’t have a capability of making music. Some of them do, but I am not the one, I am very focused I have a family, I have a band, I need my future, I need to fulfil my dream. So whatever they say, it’s not gonna stop me from doing, being the best.
Kuhusu kupungua kwa afya yake (hapa TID alikasirika kiasi cha kubadilika na kutaka kutoendelea na show)
I’m fit, I am healthy, I don’t care about what people say about me, it’s my weight, it’s my life, it’s my health. If am good, am good.
Do you think you have good healthy at the moment?
Yeah I am fine, I am healthy
I don’t think you are healthy though
Are you my doctor? Are you tryina be my doctor?
I mean you don’t look healthy
You think so but I look healthy. You haven’t taken me to hospital how do you prove such a thing? So you have a point, you brought me here today to tell me unhealthy, you wanna have an interview with an unhealthy person? I really don’t appreciate what you are saying if you are coming to the point like telling me straight I am unhealthy. I am healthy, you are not a doctor, you haven’t checked me yet so don’t tryna be.. (tusi)
Kwenye interview hiyo pia, TID alidai kuwa anatarajia kuja na filamu ya Girlfriend Part 2.
Read more: http://talkbongo.blogspot.com/2013/07/ni-kweli-kwamba-navuta-sana-bangitid.html#ixzz2YN3T49J8
CHEKI PICHA ZA KILICHOJIRI KATIKA BIRTDAY PARTY YA MSANII AY
ya :
Leo ni birthday ya mwanamuziki mchapa kazi, Ambwene Yessaya “AY” … Ni mwanamuziki wa siku nyingi akitimiza miaka kadhaa toka kuzaliwa kwake … AY aliandaliwa BASH jana usiku katika ukumbi wa Runway Lounge uliopo katika jengo la SHOPPERS PLAZA, Mikocheni Dar es Salaam.
Katika bash hiyo ambayo watu hawatasita kumpiga ndoo … “kama kawa” … ilihundhuriwa na watu kadhaa, ndugu, marafiki kama Vanessa Mdee, Eskado Bird, MwanaFA, Arthur, Mx, Sallam na wengineo …
AY anaizungumzia siku hii kuwa ni ya furaha sana, anamshukuru kila mtu aliemu-wish “HAPPY BIRTHDAY” especially kwenye mitandao ya jamii hasa twitter … Tazama baadhi ya picha katika Bash hiyo iliyoandaliwa kwa ajili ya birthday yake ;
Moet Ilifunguliwa kusheherekea AY kutumiza Miaka yake

Sallam & Vanessa
Marafiki waliokuwepo kwenye Bday party Ya AY
Moet Ilifunguliwa kusheherekea AY kutumiza Miaka yake
Subscribe to:
Posts (Atom)