Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe
ambaye alialikwa kushiriki dhifa ya Kitaifa Ikulu wakati wa ziara ya
Rais Barack Obama wa Marekani alifanya jambo kubwa muhimu kwa
mustakabali wa Demokrasia hapa nchini.
Mwenyekiti huyo ambaye pia ni
Kiongozi Rasmi wa upinzani bungeni alipata fursa adhimu ya kufanya
mazungumzo ya Faragha na maafisa wa Ikulu ya Marekani walioambatana na
Rais Barack Obama.
Mpaka sasa kilichozungumzwa na
Kiongozi huyo anayeongoza chama kinachopendwa na watanzania wengi zaidi
hakijawekwa bayana ingawa wachunguzi wa mambo wanasema yalikuwa
mazungumzo nyeti na muhimu kwa mustakabali wa demokrasia na amani ya
Tanzania.
No comments:
Post a Comment