Nashukuru Mungu siku ya leo amenijali mengi lakini baadhi yake ni pamoja na kupata muda wa kukaa na mama yangu kipenzi Bi. Sandrah. Nikiwa nyumbani na mama Diamond mama.... mama Naseeb Nyumbani.....!! Nimekuwa nipo kwenye michakato ya hapa na pale kwaajili ya kazi zangu za muziki na biashara kwa ujumla, zikiwemo na show za ndani na nje ya nchi mpaka kufikia hatua ya kutopata muda wa kukaa kitako na kuongea na mama yangu!
Siku ya leo ilikua maalum kabisa kukaa nyumbani na mama yangu kupata mawaidha mtoto. kwakuwa inafahamika siku zote mtoto kwa Mama akui'' Nimeenjoy sana kuwepo home siku nzima kudeka,kupetiwa petiwa na mama yangu na malezi kama mtoto mchanga kutoka kwake.... Kiukweli Nampenda sana Mama yangu, Hadi hapa nilipofikia namshukuru Mwenyezi Mungu.
Picha hizi Mbili ni Maalumu kuwajuza mashabiki zangu wote leo nilivyoenjoy kuwa home na mama yangu kwakua kitambo sana nilimiss kitu hii ingawa tunaonana kila siku....!! Nampenda sana Mama yangu kuliko kitu chochote duniani ingawa nina imani hata yeye ananipenda sana. Much love kwa wote wanaowapenda mama zao dunia kama mimi Binafsi navyompenda Mama yangu..!! |
No comments:
Post a Comment